Ufutuhi Katika Nyimbo Za Sherehe Za Unyago Wa Wazaramo: Utumizi Na Dhima Zake Kwa Hadhira

IKISIRI

Utafiti huu ulichunguza ujitokezaji wa ufutuhi katika nyimbo za sherehe za unyago

wa Wazaramo kwa kuangalia utumizi na dhima zake kwa hadhira. Dhana ya ufutuhi

imefasiliwa kuwa ni hali furaha, ucheshi, kicheko au tabasamu itokanayo na vijenzi

mbalimbali. Vijenzi vya ufutuhi vilivyomakinikiwa katika utafiti huu ni kejeli,

vijembe, dhihaka, na balagha.

Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani ambapo data za utafiti zilikusanywa na

baadaye kuchambuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi wa kimaelezo.

Maeneo yaliyotumika katika kukusanya data za utafiti yalikuwa ni mikoa ya Pwani,

Dar es salaam na Dodoma. Uchambuzi wa data ulizingatia misingi ya nadharia ya

Uhalisia ambayo ni; uhalisia kama mwelekeo, uhalisia kama mbinu ya kisanaa, na

uhalisia kama mbinu ya kihakiki. Nadharia hii ilisaidia kufafanua uwiano uliopo kati

ya sanaa ya uimbaji itumikayo katika sherehe za unyago wa Wazaramo na uhalisia

wa matukio ya kila siku yatokanayo na mfumo wa maisha ya jamii hii.

Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa hali ya utani, hofu na sababu za kihistoria

ndizo huwafanya Wazaramo watumie tungo za kifutuhi wakati wa sherehe za

unyago. Pia, matokeo yanabainisha kuwa Wazaramo hutumia ufutuhi katika nyimbo

za unyago wa kama kibebeo cha fikra, na hisia zinazolengwa kuwekwa wazi mbele

ya hadhira iliyokusanyika. Ufutuhi unaochopekwa katika tungo hizi huifanya hadhira

kuzing‟amua na kuzielewa kwa njia iliyojaa ucheshi, kicheko, na tabasamu. Dhamira

hizi huweza kumhusu mwali wa Kizaramo anayefanyiwa unyago, mzazi au mlezi

wake pamoja na washiriki wengine waliokusanyika katika sherehe husika.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

S., B (2021). Ufutuhi Katika Nyimbo Za Sherehe Za Unyago Wa Wazaramo: Utumizi Na Dhima Zake Kwa Hadhira. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/ufutuhi-katika-nyimbo-za-sherehe-za-unyago-wa-wazaramo-utumizi-na-dhima-zake-kwa-hadhira

MLA 8th

S., Bw. "Ufutuhi Katika Nyimbo Za Sherehe Za Unyago Wa Wazaramo: Utumizi Na Dhima Zake Kwa Hadhira" Afribary. Afribary, 25 Apr. 2021, https://afribary.com/works/ufutuhi-katika-nyimbo-za-sherehe-za-unyago-wa-wazaramo-utumizi-na-dhima-zake-kwa-hadhira. Accessed 19 Apr. 2024.

MLA7

S., Bw. . "Ufutuhi Katika Nyimbo Za Sherehe Za Unyago Wa Wazaramo: Utumizi Na Dhima Zake Kwa Hadhira". Afribary, Afribary, 25 Apr. 2021. Web. 19 Apr. 2024. < https://afribary.com/works/ufutuhi-katika-nyimbo-za-sherehe-za-unyago-wa-wazaramo-utumizi-na-dhima-zake-kwa-hadhira >.

Chicago

S., Bw. . "Ufutuhi Katika Nyimbo Za Sherehe Za Unyago Wa Wazaramo: Utumizi Na Dhima Zake Kwa Hadhira" Afribary (2021). Accessed April 19, 2024. https://afribary.com/works/ufutuhi-katika-nyimbo-za-sherehe-za-unyago-wa-wazaramo-utumizi-na-dhima-zake-kwa-hadhira