Uzingatizi Wa Viakifishi Katika Uandishi Wa Kitaaluma: Mifano Kutoka Shule Za Msingi Tanzania

SHUKURANI

Awali ya yote, ninamshukuru Mungu wangu mwenyezi kwa kunipa nguvu na kuniwezesha kukamilisha tasnifu hii. Hakika, Mungu ni mwema sana maishani mwangu. Pili, ninawashukuru wasimamizi na walimu wangu, Dkt. Rafiki Y. Sebonde na Prof. John G. Kiango, kwa mwongozo, jitihada na ushauri wao makini vilivyoniwezesha kukamilisha tasnifu hii. Hakuna awezaye kuwalipa ila Mungu pekee. Tatu, ninamshukuru sana mwalimu wangu, Prof. Hermas J.M. Mwansoko, kwa kunijengea msingi imara katika stadi za utafiti wakati akinisimamia Shahada ya Umahiri na kunihimiza kujiunga na masomo ya Shahada ya Uzamivu mapema iwezekanavyo. Halikadhalika, ninamshukuru Prof. Joshua S. Madumulla kwa ushauri wake alionipa, hasa katika hatua za mwanzo za kuchipuza wazo la kufanya utafiti katika uwanja huu wa uakifishaji. Ninakiri wazi kuwa weledi na utanashati wake wa kuandika maandiko yaliyoakifishwa vema, ulinivutia sana na kunifanya niwe mdadisi katika eneo hili. Nne, ninawashukuru wanataaluma wenzangu kwa mchango wao wa hali na mali wakati wote wa masomo yangu. Kipekee, niwashukuru Dkt. Tumaini Samweli, Dkt. Athumani S. Ponera, Dkt. Kokeli Peter, Bw. Paul Loisulie na Bi. Zuhura Badru kwa kunisomea rasimu za tasnifu hii katika hatua mbalimbali na kunipa maoni yenye tija. Tano, ninawashukuru sana babu yangu, Mzee Wilson Mkhandi na bibi yangu, Catherine Wawa, kwa kunipenda na kunitia moyo katika hatua mbalimbali nilizopita. Daima, nitamkumbuka babu yangu kwa kunikagulia madaftari yangu wakati ninasoma Shule ya Msingi iv Sita, ninawashukuru sana rafiki zangu, Alexander Kiowi, Kampuni ya NEBRIX chini ya Mkurugenzi wake Bi. Kulwa P. Mwaka na rafiki zangu wengine, Bi. Maria S. Ntui na Bwn. Nicodemus Marcel, kwa msaada wao wa hali na mali wakati wote wa kuandika tasnifu hii. Mwenyezi Mungu awabariki sana. Saba, ninawashukuru wazazi wangu, baba, Mwalimu Ogha Stephen na mama, Maria Wilson Mkhandi, kwa kunizaa, kunilea na kunisomesha. Baba yangu apumzike kwa amani. Mungu aendelee kumtunza na kumbariki mama yangu daima. Pia, ninawashukuru dada zangu na wadogo zangu wote, kwa kunitunza na kuniombea katika maisha yangu yote. Waliotangulia mbele za haki, wapumzike kwa amani. Pia, ninawashukuru wanangu wote, Elinjema, Ogha-Amani, Ogha-Brightson, OghaStephen na Esther, kwa kuniliwaza na kuniombea kila wakati. Mwisho, lakini si kwa umuhimu, ninawashukuru watu wote ambao sijawataja kwa majina kwa michango yao ya mawazo, hali na mali ambayo imefanikisha kukamilisha tasnifu hii.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Stephano, R (2021). Uzingatizi Wa Viakifishi Katika Uandishi Wa Kitaaluma: Mifano Kutoka Shule Za Msingi Tanzania. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/uzingatizi-wa-viakifishi-katika-uandishi-wa-kitaaluma-mifano-kutoka-shule-za-msingi-tanzania

MLA 8th

Stephano, Rehema "Uzingatizi Wa Viakifishi Katika Uandishi Wa Kitaaluma: Mifano Kutoka Shule Za Msingi Tanzania" Afribary. Afribary, 01 May. 2021, https://afribary.com/works/uzingatizi-wa-viakifishi-katika-uandishi-wa-kitaaluma-mifano-kutoka-shule-za-msingi-tanzania. Accessed 09 Oct. 2024.

MLA7

Stephano, Rehema . "Uzingatizi Wa Viakifishi Katika Uandishi Wa Kitaaluma: Mifano Kutoka Shule Za Msingi Tanzania". Afribary, Afribary, 01 May. 2021. Web. 09 Oct. 2024. < https://afribary.com/works/uzingatizi-wa-viakifishi-katika-uandishi-wa-kitaaluma-mifano-kutoka-shule-za-msingi-tanzania >.

Chicago

Stephano, Rehema . "Uzingatizi Wa Viakifishi Katika Uandishi Wa Kitaaluma: Mifano Kutoka Shule Za Msingi Tanzania" Afribary (2021). Accessed October 09, 2024. https://afribary.com/works/uzingatizi-wa-viakifishi-katika-uandishi-wa-kitaaluma-mifano-kutoka-shule-za-msingi-tanzania