Utanzia Katika Kasida Za Kiswahili: Mifano Kutoka Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja

SHUKRANI

Kwanza kabisa shukurani za dhati anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu ambaye ameniwezesha kufanya kazi hii kwa afya njema na nguvu nyingi. Pili, namshukuru kwa dhati mwalimu na msimamizi wangu wa utafiti huu Dkt Elias Manandi Songoyi aliyekubali au aliyejitolea kuwa mlezi na msimamizi wa kazi hii akielewa shida mbalimbali za mwanafunzi/mtoto wake kwa kunielekeza, kuniongoza, kunikosoa na kunishauri hadi kukamilika vyema tasnifu hii. Shukurani nyingine ziwaendee walimu wangu walionisomesha katika kipindi chote cha muda wa masomo, toka darasa la kwanza hadi Shahada ya Uzamili. Shukurani nyingine zimfikie Dkt Sebonde kwa kunifunza mbinu za somo hili la utafiti. Vile vile, nawashukuru walimu wangu wote wa madrasa ambao wamenifungua macho na kunionesha njia njema ya kumfuata Allah (s.w.t). Mwalimu Mwajuma Ame na Mwalimu Rajab J. Yakuti ( Mungu amlaze mahali pema peponi ) na nawashukuru sana na malipo yenu yako kwa Allah. Nawashukuru pia wazee na vijana wote niliowahoji na kukubali kuhojiwa nami pamoja na kunipa taarifa nilizozihitaji. Pia naishukuru madrasa yangu ya Arabiu Shamsiya kwa kunipa ushirikiano mkubwa katika kuwahoji. Kwani wahenga wamesema mwenda tezi na omo hurejea ngamani, nami nimerudi kwetu ili kutaka msaada. Halikadhalika nawashukuru wanafunzi wote wa kozi ya Shahada ya Uzamili katika fasihi ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dodoma wa mwaka wa 2014/2016 kwa ushirikiano wao katika masuala mbalimbali pamoja na suala zima la utafiti.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Moh‟d, H (2021). Utanzia Katika Kasida Za Kiswahili: Mifano Kutoka Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/utanzia-katika-kasida-za-kiswahili-mifano-kutoka-mkoa-wa-mjini-magharibi-unguja

MLA 8th

Moh‟d, Haruwa "Utanzia Katika Kasida Za Kiswahili: Mifano Kutoka Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja" Afribary. Afribary, 01 May. 2021, https://afribary.com/works/utanzia-katika-kasida-za-kiswahili-mifano-kutoka-mkoa-wa-mjini-magharibi-unguja. Accessed 18 Apr. 2024.

MLA7

Moh‟d, Haruwa . "Utanzia Katika Kasida Za Kiswahili: Mifano Kutoka Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja". Afribary, Afribary, 01 May. 2021. Web. 18 Apr. 2024. < https://afribary.com/works/utanzia-katika-kasida-za-kiswahili-mifano-kutoka-mkoa-wa-mjini-magharibi-unguja >.

Chicago

Moh‟d, Haruwa . "Utanzia Katika Kasida Za Kiswahili: Mifano Kutoka Mkoa Wa Mjini Magharibi Unguja" Afribary (2021). Accessed April 18, 2024. https://afribary.com/works/utanzia-katika-kasida-za-kiswahili-mifano-kutoka-mkoa-wa-mjini-magharibi-unguja