Dhima Ya Taswira Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Kwa Nasibu Abdul Na Mrisho Mpoto

IKISIRI

Tasinifu hii ni matokeo ya utafiti uliochunguza Dhima ya Taswira katika Nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya: Mifano kutoka kwa Nasibu Abdul (Diamond Platinum) na Mrisho Mpoto (Mjomba). Utafiti huu uliongozwa na malengo matatu mahsusi ambayo ni kubainisha taswira zinazojitokeza katika nyimbo za waimbaji teule, kujadili dhima ya taswira katika nyimbo za waimbaji teule na kutathmini athari za taswira katika nyimbo za waimbaji teule. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni semiotiki kupitia misingi miwili kama ilivyofafanuliwa katika utafiti huu.

Utafiti ulifanyika uwandani na maktabani. Eneo la utafiti lilihusisha mkoa wa Dodoma na Dar es salaam. Data zilikusanywa kwa njia ya uchunguzi matini na usaili ambapo sampuli ilijumuisha vijana wenye umri kati ya miaka 17 hadi 35, madijei na wanafunzi wa shahada ya kwanza katika fasihi ya kiswahili. Aidha, matini zilizochunguzwa zilihusisha nyimbo za wasanii teule ambazo kwazo taswira zilibainishwa.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa, nyimbo za waimbaji teule zimesheheni matumizi ya taswira, hivyo, kuwezesha kubainishwa kwa taswira zilizojitokeza katika nyimbo teule. Miongoni mwa taswira zinazojitokeza ni pamoja na jongoo, ngongoti, roboti, chumvi, samaki, fisi, kibakuli cha vumba, ngalawa, mwiba, kuku, chui, roho, nzi, kuni, ugali, nyumba na vyumba. Aidha, dhima tulizozibaini ni pamoja na kukwepa udhibiti, kufikisha ujumbe, kuonesha ufundi wa msanii, kuvutia hadhira, kuburudisha hadhira, na kupamba kazi ya msanii. Pia, athari chanya za matumizi ya taswira ni kuibua hisia za hadhira, hukuza udadisi wa hadhira, kukua kwa kipera husika, hufanya maudhui yaeleweka kwa urahisi na kudumisha maadili ya jamii. Na athari hasi ni pamoja na kusababisha ugumu katika kupata undani wa maudhui yanayokusudiwa, kuchochea mmomonyoko wa maadili na pia kusababisha utata wa maana. Mchango mpya wa tasinifu hii ni kuonesha dhima ya matumizi ya taswira katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya kama mbinu mojawapo ya utunzi wa kazi za kifasihi. Aidha, utafiti umependekeza tafiti nyingi zaidi ziendelee kufanyika katika eneo hili la taswira katika muziki wa kizazi kipya ili kuisheheneza zaidi fasihi simulizi ya Kiswahili.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

MGALULA, S (2021). Dhima Ya Taswira Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Kwa Nasibu Abdul Na Mrisho Mpoto. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/dhima-ya-taswira-katika-nyimbo-za-muziki-wa-kizazi-kipya-mifano-kutoka-kwa-nasibu-abdul-na-mrisho-mpoto

MLA 8th

MGALULA, SARAH "Dhima Ya Taswira Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Kwa Nasibu Abdul Na Mrisho Mpoto" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/dhima-ya-taswira-katika-nyimbo-za-muziki-wa-kizazi-kipya-mifano-kutoka-kwa-nasibu-abdul-na-mrisho-mpoto. Accessed 30 Nov. 2024.

MLA7

MGALULA, SARAH . "Dhima Ya Taswira Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Kwa Nasibu Abdul Na Mrisho Mpoto". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/dhima-ya-taswira-katika-nyimbo-za-muziki-wa-kizazi-kipya-mifano-kutoka-kwa-nasibu-abdul-na-mrisho-mpoto >.

Chicago

MGALULA, SARAH . "Dhima Ya Taswira Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya: Mifano Kutoka Kwa Nasibu Abdul Na Mrisho Mpoto" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/dhima-ya-taswira-katika-nyimbo-za-muziki-wa-kizazi-kipya-mifano-kutoka-kwa-nasibu-abdul-na-mrisho-mpoto