Fani Ya Methali Za Kisukuma Katika Uadilishaji Wa Watoto Na Vijana

IKISIRI

Utafiti huu ulihusu uchunguzi wa fani katika methali za Kisukuma katika uadilishaji wa watoto na vijana. Vipengele vya kifani vilivyochunguzwa na kuchambuliwa ni matumizi ya lugha, wahusika na mandhari. Vipengele hivyo vilichunguzwa kwa lengo la kubainisha namna mfungamano wake unavyochangia kuibua maudhui ambayo hukamilisha tendo zima la kiusemi na namna nguvu ya tendo kusudiwa inavyopokewa na watoto na vijana. Nadharia ya Tendo la Kiusemi (TELAKI) imetumika kuchanganulia vipengele hivyo. Na nadharia ya tafsiri baina ya tamaduni mbili imetumika kwa ajili ya kutafsiri methali za Kisukuma kwa Kiswahili.

Katika utafiti huu, jamii ya watafitiwa ilikuwa ni Wasukuma waishio katika maeneo ya mkoa wa Mwanza. Mbinu ya sampuli ya kitabaka ilitumika kuwapata watoto na vijana na sampuli lengwa kwa wazazi na walezi kutokana na tajiriba waliyo nayo katika matumizi ya methali. Ukusanyaji wa data ulihusisha data za uwandani na maktabani. Data zilichanganuliwa kwa njia ya mahojiano na majadiliano baina ya watafitiwa wa makundi yaliyolengwa na kuwasilishwa kwa njia ya ufafanuzi.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa maadili yaliyomo katika methali za Kisukuma yanatokana na ufungamanifu uliopo kati ya lugha, wahusika na mandhari iliyotumika kuijenga fani ya methali husika. Vipengele hivyo vya kifani ndivyo hubeba matendo kusudiwa yenye ujumbe wa aina mbalimbali unaolenga kuwajengea watoto na vijana maadili faafu katika jamii. Utafiti ulibaini pia kuwa vipengele hivyo vya fani, kwa baadhi ya methali, hutoa changamoto kwa watoto na vijana katika kuuelewa ujumbe uliokusudiwa.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Raphael, S (2021). Fani Ya Methali Za Kisukuma Katika Uadilishaji Wa Watoto Na Vijana. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/fani-ya-methali-za-kisukuma-katika-uadilishaji-wa-watoto-na-vijana

MLA 8th

Raphael, Sostenes "Fani Ya Methali Za Kisukuma Katika Uadilishaji Wa Watoto Na Vijana" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/fani-ya-methali-za-kisukuma-katika-uadilishaji-wa-watoto-na-vijana. Accessed 03 May. 2024.

MLA7

Raphael, Sostenes . "Fani Ya Methali Za Kisukuma Katika Uadilishaji Wa Watoto Na Vijana". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 03 May. 2024. < https://afribary.com/works/fani-ya-methali-za-kisukuma-katika-uadilishaji-wa-watoto-na-vijana >.

Chicago

Raphael, Sostenes . "Fani Ya Methali Za Kisukuma Katika Uadilishaji Wa Watoto Na Vijana" Afribary (2021). Accessed May 03, 2024. https://afribary.com/works/fani-ya-methali-za-kisukuma-katika-uadilishaji-wa-watoto-na-vijana