IKISIRI
Tasnifu hii inahusu Mabadiliko ya Vionjo vya Kiuandishi katika Riwaya ya Kiswahili.
Utafiti ulijigeza katika kulinganisha na kulinganua mabadiliko hayo katika riwaya za
Shaaban Robert na Said A. Mohamed. Neno vionjo katika tasnifu hii limetumika kama
hali ya kimajaribio au mwondoko wa utanzu fulani wa Fasihi kutoka sura iliyozoeleka
kwenda sura mpya ambayo haijazoeleka. Mtafiti ameamua kuchunguza mabadiliko ya
vionjo vya kiuandishi katika riwaya ya Kiswahili kwa sababu, kwa kiasi kikubwa bado
dhana hii ya mabadiliko ya vionjo vya kiuandishi haijafanyiwa uchunguzi.
Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktabani tuliyadurusu mapitio mbalimbali
kama vile majarida, tasnifu, tahakiki, makala na vitabu. Uwandani tulitumia mbinu ya
mahojiano ili kupata data za utafiti wetu. Utafiti ulitumia nadharia ya uhalisia ambayo
humtaka mtunzi kutunga kwa kuzingatia suala la wakati pamoja na kujua historia ya jamii
husika. Mabadiliko haya katika riwaya ya Kiswahili yanazingatia pia vitu hivyo.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa uandishi wa riwaya ya Kiswahili umebeba
mabadiliko kadhaa katika uandishi wake. Mabadiliko haya katika vionjo vya kiuandishi
yanachangiwa sana na vitu kama vile mabadiliko ya kijamii (historia za jamii),
umajaribio, ongezeko la wasomi na hata maendeleo ya sayansi na tekinolojia kwa kiasi
kikubwa. Mchango mpya wa tasnifu hii ni kuonesha vionjo vinavyotumiwa na waandishi
mbalimbali katika utunzi hasa katika riwaya ya Kiswahili.
Jumanne, A (2021). Mabadiliko Ya Vionjo Vya Kiuandishi Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Shaaban Robert Na Said A. Mohamed. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/mabadiliko-ya-vionjo-vya-kiuandishi-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-shaaban-robert-na-said-a-mohamed
Jumanne, Arafa "Mabadiliko Ya Vionjo Vya Kiuandishi Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Shaaban Robert Na Said A. Mohamed" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/mabadiliko-ya-vionjo-vya-kiuandishi-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-shaaban-robert-na-said-a-mohamed. Accessed 30 Nov. 2024.
Jumanne, Arafa . "Mabadiliko Ya Vionjo Vya Kiuandishi Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Shaaban Robert Na Said A. Mohamed". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/mabadiliko-ya-vionjo-vya-kiuandishi-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-shaaban-robert-na-said-a-mohamed >.
Jumanne, Arafa . "Mabadiliko Ya Vionjo Vya Kiuandishi Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganisho Wa Riwaya Za Shaaban Robert Na Said A. Mohamed" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/mabadiliko-ya-vionjo-vya-kiuandishi-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganisho-wa-riwaya-za-shaaban-robert-na-said-a-mohamed