Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa

IKISIRI

Utafiti ulichunguza matumizi ya lugha katika methali kwa kujiegemeza katika

methali za Kinyakyusa kama mfano. Methali kama utanzu wa Fasihi Simulizi wenye

hekima unaoeleza kwa ufasaha wa lugha kwa ufupi wenye kufurahisha, una

umuhimu sana katika jamii katika kuelimisha. Kipengele hiki hakijatafitiwa kwa kina

katika methali za Kinyakyusa.

Taarifa za utafiti huu zilikusanywa kwa njia ya usaili, dodoso na mjadala wa kikundi

katika mkoa wa Mbeya wilaya ya Kyela. Uchunguzi wa taarifa za utafiti

zilizokusanywa uliongozwa na nadharia ya Umuundo ambayo ni miongoni mwa

nadharia za uhakiki wa kazi za Fasihi inayochambua kazi ya Fasihi kwa kuichunguza

kazi yenyewe. Uchambuzi wa data ulifanyika kwa njia ya ufafanuzi.

Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba matumizi ya methali katika jamii ya

Bhanyakyusa yameanza kupotea kutokana na muingiliano mkubwa na jamii

zinazotumia lugha tofauti na Kinyakyusa. Pia, imedhihirika kuwa uteuzi wa maneno

yanayotumika katika methali huzingatia dhima ya methali inayotambwa katika

kujenga picha na ishara kwa jamii. Aidha, utafiti huu umebaini kuwa methali za

lugha ya Kinyakyusa zinapotumiwa miongoni mwa wanajamii kunakuwepo na athari

chanya kwa wamilisi wa lugha hiyo; pamoja na athari hasi kwa wale wasio na umilisi

wa kutosha juu ya lugha hiyo. Jambo hili linahatarisha kupotea kwa matumizi ya

utanzu huu miongoni mwa Bhanyakyusa.

Utafiti huu una mchango mkubwa katika taaluma ya Fasihi Simulizi kwani ni

sehemu ya kutunza amali za jamii. aidha, unatoa changamoto kwa watafiti

kujishughulisha na methali na Fasihi Simulizi kwa ujumla ili kuiepusha na upotevu

unaotokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Philip, D (2021). Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa

MLA 8th

Philip, Daud "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa. Accessed 30 Nov. 2024.

MLA7

Philip, Daud . "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa >.

Chicago

Philip, Daud . "Matumizi Ya Lugha Katika Methali: Mfano Katika Methali Za Kinyakyusa" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/matumizi-ya-lugha-katika-methali-mfano-katika-methali-za-kinyakyusa