Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla

IKISIRI

Tasnifu hii inahusu Matumizi ya msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari

katika riwaya za Muhammed Said Abdulla. Msamiati ni jumla ya maneno

yaliyomo katika lugha. Hivyo, kwa mujibu wa utafiti huu maneno yenyewe

yalichunguzwa kupitia riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale, Duniani Kuna Watu na

Kosa la Bwana Msa. Uchunguzi huu ulilenga kuchunguza na kubainisha msamiati

huo na etimolojia yake pamoja na athari yake kwa wasomaji.

Sababu ya kuchunguza suala hilo lilitokana na mtafiti kuvutika na lugha ya utunzi

wa riwaya hizo. Shabaha ni kupunguza au kuondoa tatizo la kutofahamika maana

iliyokusudiwa kwa baadhi ya msamiati, hasa kwa wale ambao si weledi wa kucheza

na lugha hiyo.

Mbinu ambazo zilitumika kupata data ni udurusu wa maandiko, udodosaji na

mahojiano. Jamii tafitiwa katika uchunguzi huu ilikuwa ni ya Wazanzibari kwa kuwa

ndiyo jamii ya mtunzi wa riwaya hizo. Data za uwandani zilizopatikana kwao

zilichanganywa na zile za maktabani kupitia maandiko mbalimbali. Data hizi

zilihusishwa na nadharia ya uhalisia kuhusu upatikanaji wa etimolojia sahihi ya

msamiati unaosawiri mazingira ya Kizanzibari na matukio ambayo yamo katika

riwaya za mtunzi huyo ambayo yamekithiri msamiati huo.

Matukio ya uchunguzi huo yalibaini kuwa usawiri wa msamiati na mazingira ya

Kizanzibari katika riwaya za Muhammed Said Abdulla upo kwa kiwango kikubwa.

Usawiri huo ulibainika zaidi kupitia miktadha ya maisha ya Wazanzibari kijiografia,

kilugha, kisanaa na kiutamaduni. Aidha, msamiati uliobainika ulijikita katika

vipengele vya kihistoria (kupitia lugha ya Kiarabu na Kiingereza), kiutamaduni

(kupitia utamaduni wa dini ya Kiislamu), na kilahaja (kupitia vijilugha vya wakazi

wa Zanzibar). Hali hiyo imetoa athari kwa wasomaji ya kuvutika na uandishi wa

mtunzi huyo, kubaini historia na silika yake, kubaini umahiri wake wa matumizi ya

visawe, kubaini historia na athari ya Wakoloni, kutambulisha lahaja na utofauti wake

kimatumizi, kushajiisha matumizi ya msamiati uliopo hatarini kupotea, na kuathiri

watunzi wengine wa Zanzibar waliomfuatia. Pia matokeo ya uchunguzi huo yametoa

mchango mpya kwa kuorodhesha msamiati na asili zake katika riwaya hizo.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Said, S (2021). Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla

MLA 8th

Said, Saida "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla. Accessed 30 Nov. 2024.

MLA7

Said, Saida . "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla >.

Chicago

Said, Saida . "Matumizi Ya Msamiati Unaosawiri Mazingira Ya Kizanzibari Katika Riwaya Za Muhammed Said Abdulla" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/matumizi-ya-msamiati-unaosawiri-mazingira-ya-kizanzibari-katika-riwaya-za-muhammed-said-abdulla