Matumizi Ya Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Ulinganisho Wa Diwani Za Mathias Mnyampala Na Amri Abedi Kaluta

IKISIRI

Utafiti huu unahusu matumizi ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili: Ulinganisho wa diwani za Mathias Mnyampala na Amri Abedi Kaluta. Ujaala ni falsafa ambayo hutawala na kuongoza maisha ya binadamu (Ponera, 2014). Falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili haijatafitiwa vya kutosha hivyo, kuwanyima fursa wasomaji na watunzi wa kazi za fasihi na kutoelewa dhana ya ujaala. Hii imemsukuma mtafiti kuchunguza matumizi ya falsafa ya ujaala katika ushairi wa Kiswahili.

Kwa kiasi kikubwa, utafiti huu ulifanyika maktabani, baadaye mtafiti alienda uwandani kufanya mahojiano na wataalamu pamoja na familia za waandishi teule. Kwa mintarafu hiyo, mkabala wa kitaamuli ndio uliotumika katika uwasilishaji wa data za utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulitumia nadharia ya udhanaishi kutokana na kuakisi kwake suala la kuamini katika uwepo wa Mungu kama inavyojidhihirisha katika diwani za waandishi teule zilizotumika katika utafiti huu.

Matokeo ya utafiti huu yamebaini kuwa, katika ushairi wa Kiswahili kuna matumizi makubwa ya falsafa ya ujaala. Matumizi hayo hufanana na kutofautiana miongoni mwa waandishi teule waliotumika katika kazi hii. Kuna mpishano mkubwa baina ya jamii moja na nyingine. Licha ya mpishano huo, wote huamini katika kani ya Mungu inayotawala na kuongoza maisha ya binadamu. Utatifi huu uliibua michango mipya mbalimbali. Utafiti huu umependekeza tafiti zaidi zifanyike juu ya matumizi ya ujaala katika riwaya na tamthilia.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

MBWAMBO, G (2021). Matumizi Ya Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Ulinganisho Wa Diwani Za Mathias Mnyampala Na Amri Abedi Kaluta. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/matumizi-ya-ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-ulinganisho-wa-diwani-za-mathias-mnyampala-na-amri-abedi-kaluta

MLA 8th

MBWAMBO, GRACE "Matumizi Ya Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Ulinganisho Wa Diwani Za Mathias Mnyampala Na Amri Abedi Kaluta" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/matumizi-ya-ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-ulinganisho-wa-diwani-za-mathias-mnyampala-na-amri-abedi-kaluta. Accessed 30 Nov. 2024.

MLA7

MBWAMBO, GRACE . "Matumizi Ya Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Ulinganisho Wa Diwani Za Mathias Mnyampala Na Amri Abedi Kaluta". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/matumizi-ya-ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-ulinganisho-wa-diwani-za-mathias-mnyampala-na-amri-abedi-kaluta >.

Chicago

MBWAMBO, GRACE . "Matumizi Ya Ujaala Katika Ushairi Wa Kiswahili: Ulinganisho Wa Diwani Za Mathias Mnyampala Na Amri Abedi Kaluta" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/matumizi-ya-ujaala-katika-ushairi-wa-kiswahili-ulinganisho-wa-diwani-za-mathias-mnyampala-na-amri-abedi-kaluta