IKISIRI
Fasihi ni kioo cha jamii. Fasihi imekuwepo tangu jadi. Fasihi hunuia kufunza mada kuu katika jamii kama vile; mila, itikadi, dini, miiko, imani, matambiko, tamaduni za kale, utawala na kadhalika. Mambo haya yana nguvu mahsusi katika jamii. Fasihi kama katiba yoyote ile, huelimisha, huhifadhi tamaduni na pia kuburudisha. Utafiti huu ulilenga kuchunguza na kutathmini nafasi na athari ya kiongozi wa kike katika tamthilia teule za Kiswahili. Tamthilia ikiwa utanzu mmojawapo wa fasihi andishi ziliteuliwa ili kutufaa. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuchanganua dhana ya uhusika katika tamthilia husika. Tulipambanua na kuchanganua nafasi ya viongozi wa kike na tukatoa tathmini ya athari yao kwa kuwasilisha sifa zao na mwelekeo wao katika jamii husishi. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Ufeminsti wa Kiafrika. Hali lengwa halisi ni ya jamii nyingi za bara za Afrika kihadhi na kitamaduni. Katika kuendeleza utafiti huu tulitumia mbinu kusudio ili kuteua tamthilia za Kilio cha Haki, Posa za Bikisiwa, Sudana na Pango. Njia ya ukusanyaji data ilikuwa ya kuhakiki matini. Data iliyopatikana ilichanganuliwa kwa kuzingatia malengo, maswali na nadharia ya utafiti na matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti huu utasaidia kuelewa nafasi na athari ya kiongozi wa kike kwa mujibu wa waandishi watukuka katika Kiswahili. Masuala ya kimsingi ya utafiti yalilengwa sawasawa. Utafiti huu pia uliangazia dhana ya uhusika, uteuzi wa wahusika kutoka tamthilia teule na muhtasari wa tamthilia zilizofaa utafiti huu. Uchunguziwa kina wa nafasi chanya na hasi ya kiongozi wa kike ulifanywa. Uchanganuzi wa athari na changamoto zinazomkabili kiongozi wa kike ulishughulikwa.Hatimaye muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti wetu ulifikiwa.Utafiti wetu vilevile ulinufaika kutoka kwa marejeleo mbalimbali vitabuni na wavuti tuliyoyapitia ili kukusanya data iliyolenga mada ya utafiti. Dhamira kuu ya utafiti huu ililenga ushirikiano, uana na suala zima la mapinduzi ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi. Utafiti huu ulizamia mada ya utafiti kwa kina ili kufikia upeo wa juu katika utafiti, daraja ya uzamili. Matokeo yatakuwa na mchango mkubwa katika fasihi ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla.
NYANGWESO, S (2021). Nafasi Na Athari Ya Kiongozi Wa Kike Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/nafasi-na-athari-ya-kiongozi-wa-kike-katika-tamthilia-teule-za-kiswahili
NYANGWESO, SYEKEI "Nafasi Na Athari Ya Kiongozi Wa Kike Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili" Afribary. Afribary, 07 May. 2021, https://afribary.com/works/nafasi-na-athari-ya-kiongozi-wa-kike-katika-tamthilia-teule-za-kiswahili. Accessed 18 Dec. 2024.
NYANGWESO, SYEKEI . "Nafasi Na Athari Ya Kiongozi Wa Kike Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili". Afribary, Afribary, 07 May. 2021. Web. 18 Dec. 2024. < https://afribary.com/works/nafasi-na-athari-ya-kiongozi-wa-kike-katika-tamthilia-teule-za-kiswahili >.
NYANGWESO, SYEKEI . "Nafasi Na Athari Ya Kiongozi Wa Kike Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili" Afribary (2021). Accessed December 18, 2024. https://afribary.com/works/nafasi-na-athari-ya-kiongozi-wa-kike-katika-tamthilia-teule-za-kiswahili