Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed

IKISIRI

Tasnifu hii inahusu suala la malezi ya mtoto wa kike katika riwaya ya Kiswahili

ambayo ni miongoni mwa kazi za Fasihi Andishi zilizomakinikia jambo hili.

Tumepata kariha ya kufanya utafiti huu baada ya kuona kwamba kipengele cha

malezi ya mtoto wa kike, licha ya kusawiriwa katika riwaya ya Kiswahili,

hakijachunguzwa vya kutosha, huku mtoto wa kike akikabiliwa na changamoto

mbalimbali za kimalezi na kimazingira hasa katika zama hizi za utandawazi. Pia,

wazazi na walezi wanaonekana kukabiliwa na changamoto anuwai katika kuwalea

watoto wao wa kike.

Utafiti uliongozwa na malengo manne; kuchunguza mikitadha ya maisha ya

waandishi teule na athari zake katika kusawiri malezi ya mtoto wa kike, mifumo ya

malezi ya mtoto wa kike katika jamii za waandishi teule, kuwapo au kutokuwapo

kwa upatanifu wa vipengele vya malezi ya mtoto wa kike katika riwaya na maisha ya

jamii za waandishi teule, na kulandana na kutofautiana kwa vionjo vya malezi ya

mtoto wa kike katika riwaya teule za waandishi teule.

Data za msingi tulizipata kwa kudurusu riwaya teule, na fuatizi tulizipata uwandani

kupitia njia za udodosi, na mahojiano. Tumefanya utafiti katika mikoa ya Kaskazini

Pemba, Mjini Magharibi (Unguja), Mwanza, Dodoma, Dar es Salaam na Tanga.

Nadharia tuliyoitumia katika utafiti huu wa kifafanuzi ni ya Ufeministi sambamba na

mkabala wake wa Ufeministi wa ki-Afrika, ilituongoza katika kukusanya na

kuchanganua data.

Elimu ya malezi inahitajika kwa wazazi na walezi ili malezi kwa watoto wakiwamo

wa kike, yaendane na mabadiliko katika jamii ya sasa.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

Mohamedi, R (2021). Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed

MLA 8th

Mohamedi, Rasuli "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed" Afribary. Afribary, 27 Apr. 2021, https://afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed. Accessed 06 May. 2024.

MLA7

Mohamedi, Rasuli . "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed". Afribary, Afribary, 27 Apr. 2021. Web. 06 May. 2024. < https://afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed >.

Chicago

Mohamedi, Rasuli . "Suala La Malezi Ya Mtoto Wa Kike Katika Riwaya Ya Kiswahili: Ulinganishi Wa Riwaya Za E. Kezilahabi Na S. A. Mohamed" Afribary (2021). Accessed May 06, 2024. https://afribary.com/works/suala-la-malezi-ya-mtoto-wa-kike-katika-riwaya-ya-kiswahili-ulinganishi-wa-riwaya-za-e-kezilahabi-na-s-a-mohamed

Document Details
Rasuli Mohamedi Field: Linguistics Type: Thesis 162 PAGES (36936 WORDS) (pdf)