Tathmini Ya Matumizi Ya Vifaa Vya Kufundishia Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Zamsingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya

IKISIRI

Utafiti huu ulishughulikia uchunguzi wa matumizi ya vifaa vya ufundishaji wa msamiati wa Kiswahili katika shule za msingi za umma, Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki, Kenya. Madhumuni aliyozingatia mtafiti katika utafiti huu yalikuwa ni pamoja na kutambua changamoto zilizopo wakati wa kutumia vinyago, video na chati katika somo la msamiati, pili ni kudadisi sera zilizopo za ukaguzi ili kudhibiti matumizi wa video, chati na vinyago ili kusaidia uelewekaji wa misamiati na kuchunguza udhaifu na ufaafu uliopo katika ufundishaji msamiati kwa kutumia video, chati na vinyago katika somo la Kiswahili.Utafiti ulifanywa katika shule kumi za Kisumu Mashariki. Hojaji zilitumika kukusanya data ya walimu mkuu, walimu wa Kiswahili.Nakala ya uchunguzi somo ya walimu wa Kiswahili ilitumika .Uteuzi wa sampuli ya wanafunzi ,walimu wa Kiswahili ilikuwa ya unasibu na sampuli kusudi kwani walengwa hawa ndio walikuwa na vigeu ambavyo mtafiti alihitaji.Data ilikusanywa kwa vifaa hivi vya utafiti,nakala ya uchunguzi na hojaji.Utafiti awali ulifanyika ili udhabiti na uthamni upatikane kabla utafiti halisi, ili kurekebisha kasoro .Mbinu iliyotumika ya kushughulikia utafiti ni kwanza kuteua kichwa,uteuzi wa shule husika ,walengwa wa utafiti ,njia za kukusanya data,kuchanganua data,,kudhibiti na kudhamni vifaa ili kurekebisha makosa kabla ya utafito wenyewe. Utafiti ulidhibitisha somo lenye vifaa hufurahiwa,huvutia hisia ,hurahisisha uelewa wa dhana, hivyo kuboresha matokeo ya mtihani.Utafiti ulilenga idadi ya walimu kumi wa Kiswahili katika Shule za msingi katika Kaunti ya Kisumu Mashariki.Mtafiti aliteua sampuli kwa bahati nasibu. Walengwa walioteuliwa walikuwa walimu wakuu kumi, walimu wa Kiswahili kumi na wanafunzi kumi. Walengwa wote walikuwa mia nane ishirini ambao walikuwa asilimia kumi, basi idadi iliyohojiwa ikawa themanini na mbili . Hojaji zilikuwa aina tatu: za walimu wakuu, walimu wa Kiswahili na wanafunzi. Utafiti ulichanganulia kwa kutumia kifaa cha uchanganuzi data( SPSS) kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi. Baada ya kutafiti na kuchanganua data, mtafiti alipendekeza kuwa, kuna haja ya walimu wa Kiswahili kuwa na vikao katika majopoili wajadiliane na kutayarisha visaidizi wanavyohitaji ili kuboresha ufunzaji na uelewekaji wa msamiati. Pamoja na hayo,walimu wanahitaji kuunda sera za kutengeneza visaidizi vya somo la Kiswahili zitakazowawezesha kupanga mikakati ya kukaguana wao kwa wao. Jambo hili litakuza umoja wa kufaana. Mtafiti pia alionelea kuwa kuna haja ya washika dau wote wa elimu kufufua taasisi za Kaunti ili kukuza hitaji la uundaji visaidizi ili walimu waendeleze weledi wao wa kuunda visaidizi ili kuboresha uelewekaji wa dhana za Kiswahili. Kadhalika,washika dau wana changamoto kubwa ya kuleta mashuleni rasilimali za kutosha kutengeneza visaidizi vinavyohitajika. Jambo lingine ni kuwa shulezitengesehemu mahususi za kuhifadhi visaidizi ili vitumike bila uwoga wa kuharibika ama kupotea. Mwisho, walimu waweke misingi thabiti ya ufunzaji msamiati kuanzia madarasa ya chini ili wanafunzi wazielewe dhana hizi kimakosa, kisha pawe na hitaji kuzirekebisha baadaye.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

WAMBUI, K (2021). Tathmini Ya Matumizi Ya Vifaa Vya Kufundishia Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Zamsingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/tathmini-ya-matumizi-ya-vifaa-vya-kufundishia-msamiati-wa-kiswahili-katika-shule-zamsingi-za-umma-kaunti-ya-kisumu-mashariki-kenya

MLA 8th

WAMBUI, KAMAU "Tathmini Ya Matumizi Ya Vifaa Vya Kufundishia Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Zamsingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya" Afribary. Afribary, 01 Jun. 2021, https://afribary.com/works/tathmini-ya-matumizi-ya-vifaa-vya-kufundishia-msamiati-wa-kiswahili-katika-shule-zamsingi-za-umma-kaunti-ya-kisumu-mashariki-kenya. Accessed 04 Nov. 2024.

MLA7

WAMBUI, KAMAU . "Tathmini Ya Matumizi Ya Vifaa Vya Kufundishia Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Zamsingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya". Afribary, Afribary, 01 Jun. 2021. Web. 04 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/tathmini-ya-matumizi-ya-vifaa-vya-kufundishia-msamiati-wa-kiswahili-katika-shule-zamsingi-za-umma-kaunti-ya-kisumu-mashariki-kenya >.

Chicago

WAMBUI, KAMAU . "Tathmini Ya Matumizi Ya Vifaa Vya Kufundishia Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Zamsingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya" Afribary (2021). Accessed November 04, 2024. https://afribary.com/works/tathmini-ya-matumizi-ya-vifaa-vya-kufundishia-msamiati-wa-kiswahili-katika-shule-zamsingi-za-umma-kaunti-ya-kisumu-mashariki-kenya

Document Details
KAMAU HELLEN WAMBUI Field: Linguistics Type: Thesis 98 PAGES (18514 WORDS) (pdf)