IKISIRI
Shughuli nyingi za kijamii hutumia lugha inayopata maana katika muktadha
inamotumika. Hali hii imechochea kutaka kujua namna Waisukha wanavyotumia lugha
kuendeleza ubabedume katika majigambo yanayoghaniwa kwenye sherehe za
upiganishaji fahali kisemantiki. Utafiti huu ulichunguza ubabedume miongoni mwa
Waisukha jinsi unavyodhihirika katika Majigambo ya Miviga ya Shilembe na Mchezasili
wa Mayo. Vipashio vya lugha vinavyosheheni ubabedume katika majigambo hayo
vilihakikiwa kwa mtazamo wa kisemantiki. Utafiti uliongozwa na madhumuni haya:
kupambanua vipashio vya lugha hususan nomino, vishazi na vitenzi katika majigambo ya
miviga ya Shilembe na Mchezasili wa Mayo vinavyodhihirisha ubabedume miongoni
mwa Waisukha kisemantiki, kuhakiki tamathali za usemi zinazosheheni ubabedume kwa
mtazamo wa kisemantiki na kutalii nafasi ya lugha, historia na itikadi za Waisukha katika
kujenga na kudumisha ubadedume. Utafiti huu uliongozwa na nadharia mbili: Nadharia
ya UCHAMAWADI na Uwezo-Uume. Wachangiaji mashuhuri katika nadharia ya
UCHAMAWADI ni wataalam kama vile; Gee (1990), Fairclough (1992), Teun Van Dijk
(1993) na Wodak (2001). Iliwekewa msingi na kazi mbalimbali za wataalam hawa.
Hutambua uamilifu wa lugha katika jamii. Mihimili yake mikuu ni; uhakiki, uwezo au
mamlaka, historia na itikadi. Nadharia ya Uwezo-Uume iliasisiwa na Robert Bly (Well &
Holland, 2001) na kuendelezwa na Connell (1995). Inahusisha mahusiano ya wanawake
na wanaume katika jamii. Baadhi ya mihimili yake ni; itikadi za kijamii ambazo
huongoza fikra, mitazamo na mielekeo ya wanajamii kuhusu hali mbalimbali za kijamii.
Nadharia hizi zilitumiwa ili kuchangiana. Utafiti huu ulifanywa katika Kaunti Ndogo ya
Shinyalu, Kaunti ya Kakamega. Watafitiwa walikuwa fanani na washiriki katika sherehe
za Shilembe na Mchezasili wa Mayo. Usampulishaji ulifanywa kwa kutumia aina tatu.
Utafiti ulilenga kukusanya majigambo ishirini na saba kimaksudi kutegemea nasaba
ishirini na saba za Waisukha. Majigambo kumi na sita yalikusanywa kwa kutumia uteuzi
wa kimapokezano. Uteuzi wa kimaksudi ulitumiwa kuteua nasaba saba zilizo na
majigambo maarufu na uteuzi wa kinasibu ukatumiwa kuchagua majigambo tisa. Jumla
ya majigambo yaliyotumiwa yalikuwa kumi na sita. Mbinu za Uchunzaji-Shiriki na
Kiethnografia zilitumiwa na zilijumuisha kuishi na watafitiwa, kushiriki, kushuhudia
sherehe hizo pamoja na kuwahoji ili kukusanya majigambo hayo.Data iliwasilishwa na
kuchanganuliwa kupitia maelezo ya kifafanuzi na mifano, picha na vielelezo. Matokeo
yamebainisha kuwa, lugha ni kipengele muhimu cha jamii ya Waisukha kwa vile
humsawiri mwanamume Mwisukha kama aliye na mamlaka zaidi ya mwanamke. Hali hii
itafaidi jinsia ya kike kwa vile wanaume watayashughulikia majukumu yao kikamilifu
katika jamii. Utafiti umebainisha kuwa, uwezo wa mwanaume umetamalaki katika
majigambo ya Waisukha yaliyosheheni vipashio vya lugha kisemantiki. Unatarajiwa
kuupanua uwanja wa Fasihi Simulizi na Isimu kwa kulikuza suala la kuchanganua
majigambo, kipera ambacho ni muhimu katika Fasihi Simulizi kwa mtazamo wa
kisemantiki. Utafiti unatoa mchango katika kuelewa umuhimu wa Shilembe na
Mchezasili wa Mayo na mila, desturi na itikadi za Waisukha zinazowasilishwa kutoka
kizazi kimoja hadi kingine kupitia masimulizi ya Mwafrika.Utafiti huu unanuia
kuwachochea wasomi wa Fasihi Simulizi na Isimu wa baadaye kuchanganua Fasihi
Simulizi kwa kina zaidi kwa kuangazia vipashio vya lugha na kuzua
mwingilianotaaluma katika Kiswahili.
, K & Lukamika, M (2021). Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki
, Kibigo and Mary Lukamika "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki" Afribary. Afribary, 07 May. 2021, https://afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki. Accessed 18 Dec. 2024.
, Kibigo, Mary Lukamika . "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki". Afribary, Afribary, 07 May. 2021. Web. 18 Dec. 2024. < https://afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki >.
, Kibigo and Lukamika, Mary . "Ubabedume Katika Majigambo Ya Miviga Ya Shilembe Na Mchezasili Wamayomiongoni Mwa Waisukha Nchini Kenya Kwa Mtazamo Wa Kisemantiki" Afribary (2021). Accessed December 18, 2024. https://afribary.com/works/ubabedume-katika-majigambo-ya-miviga-ya-shilembe-na-mchezasili-wamayomiongoni-mwa-waisukha-nchini-kenya-kwa-mtazamo-wa-kisemantiki