Uchanganuzi Na Uhakiki Wa Athari Za Unukuzi-Hati Kutoka Kiarabu Kwenda Kiswahili – Mifano Kutoka Utenzi Wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah A. Nasir – Tafsiri Ya William Hichens 1939)

IKISIRI

Utafiti huu umejikita katika mada ya Uchanganuzi na Uhakiki wa Athari za Unukuzi-hati kutoka Kiarabu kwenda Kiswahili – Mifano kutoka Utenzi wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah bin Nasir – Tafsiri ya William Hichens 1939). Kwa asili ya Utenzi wa Al-Inkishafi uliandikwa kwa Hati ya Kiarabu katika lugha ya Kiswahili. Utenzi huo umekuwa ni ufunguo wa utafiti huu kutokana na kuwa na sifa ya historia ndefu iliyobeba istilahi zilizosheheni mitazamo ya kitafiti kati ya Hati ya Kiarabu na Hati ya Kirumi zilizochangia maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Mmsingi wa utafiti huu upo mambo yafuatayokwanza, suala kuu la utafiti huu ni kuwa hapajawahi kutafitiwa athari zilizojitokeza katika taaluma hii ya Unukuzi-hati na nafasi yake au mchango wake katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Pili,mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni kutumia tasnia ya Unukuzi zaidi kama vile; Unukuzi-hati1, ambayo ndiyo ilikuwa mwongozo mkubwa kwa kupitia kazi za wataalamu waliotangulia, na kisha kuunganisha mitazamo yao ikiongozwa na Nadharia ya Unyambuaji Vitenzi. Mbinu nyingine ni ile ya mahojiano na udodosaji kwa watafitiwa. Tatu, utafiti huu ulichunguza na kuchanganua kwa makini athari ya Hati Chanzi ya Kiarabu kwenda katika Hati Lengwa ya Kirumi (ambayo ndiyo inayotumiwa katika lugha ya Kiswahili). Utenzi wa Al-Inkishafi uliteuliwa kama ni mfano muhimu wa uchanganuzi na Uhakiki wa Athari za Unukuzi-hati.

Matokeo ya utafiti huu yana manufaa ya kuihuisha taaluma ya Unukuzi-hati, ambayo inaonekana kutopewa kipaumbele kutokana na sababu kubwa ya matumizi ya lugha zaidi ya mbili au tatu,. Pia, utafiti huu umependekeza njia nyepesi ya wasomi wengi kujifunza mbinu za Unukuzi-hati. Aidha, utafiti umeweza kuonesha asili ya mabadiliko ya hati hizi mbili (Kiarabu na Kirumi) kwa kurejelea na kuzingatia Etimolojia na Filolojia yake. Pia umeweza kuhamasisha na kutoa nafasi ya watafiti wengine kuchunguza njia za Unukuzi-hati nyingine kama vile Kiajemi, Kichina, Kikorea na Kihindi, ili wabaini michango ya lugha hizo katika ujenzi wa hati kwenda katika hati lengwa ya Kirumi.

Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

FERUZI, A (2021). Uchanganuzi Na Uhakiki Wa Athari Za Unukuzi-Hati Kutoka Kiarabu Kwenda Kiswahili – Mifano Kutoka Utenzi Wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah A. Nasir – Tafsiri Ya William Hichens 1939). Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/uchanganuzi-na-uhakiki-wa-athari-za-unukuzi-hati-kutoka-kiarabu-kwenda-kiswahili-mifano-kutoka-utenzi-wa-al-inkishafi-na-sayyid-abdallah-a-nasir-tafsiri-ya-william-hichens-1939

MLA 8th

FERUZI, ABDUL "Uchanganuzi Na Uhakiki Wa Athari Za Unukuzi-Hati Kutoka Kiarabu Kwenda Kiswahili – Mifano Kutoka Utenzi Wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah A. Nasir – Tafsiri Ya William Hichens 1939)" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/uchanganuzi-na-uhakiki-wa-athari-za-unukuzi-hati-kutoka-kiarabu-kwenda-kiswahili-mifano-kutoka-utenzi-wa-al-inkishafi-na-sayyid-abdallah-a-nasir-tafsiri-ya-william-hichens-1939. Accessed 26 Jan. 2025.

MLA7

FERUZI, ABDUL . "Uchanganuzi Na Uhakiki Wa Athari Za Unukuzi-Hati Kutoka Kiarabu Kwenda Kiswahili – Mifano Kutoka Utenzi Wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah A. Nasir – Tafsiri Ya William Hichens 1939)". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 26 Jan. 2025. < https://afribary.com/works/uchanganuzi-na-uhakiki-wa-athari-za-unukuzi-hati-kutoka-kiarabu-kwenda-kiswahili-mifano-kutoka-utenzi-wa-al-inkishafi-na-sayyid-abdallah-a-nasir-tafsiri-ya-william-hichens-1939 >.

Chicago

FERUZI, ABDUL . "Uchanganuzi Na Uhakiki Wa Athari Za Unukuzi-Hati Kutoka Kiarabu Kwenda Kiswahili – Mifano Kutoka Utenzi Wa Al-Inkishafi (Na Sayyid Abdallah A. Nasir – Tafsiri Ya William Hichens 1939)" Afribary (2021). Accessed January 26, 2025. https://afribary.com/works/uchanganuzi-na-uhakiki-wa-athari-za-unukuzi-hati-kutoka-kiarabu-kwenda-kiswahili-mifano-kutoka-utenzi-wa-al-inkishafi-na-sayyid-abdallah-a-nasir-tafsiri-ya-william-hichens-1939