Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi

IKISIRI

Utafiti huu umechunguza ufumbaji katika riwaya mbili za Katama Mkangi: Mafuta na

Walenisi. Utafiti huu umelenga: Kwanza, kubainisha aina mbalimbali za ubunifu wa

ufumbaji uliojitokeza katika riwaya ya Mafuta na Walenisi. Pili, kudhihirisha jinsi ufumbaji

ulivyotumiwa na mwandishi kama kichocheo cha zinduko katika riwaya ya Mafuta na

Walenisi. Tatu, kudhihirisha namna ufumbaji umeendeleza au kukwamiza usawiri wa

wahusika wa mtunzi. Nne, kutathimini jinsi mazingira ya mwandishi yalivyochangia

matumizi ya mafumbo katika riwaya ya Mafuta na Walenisi. Utafiti huu umebainisha kuwa,

wakati ambapo Mkangi alikuwa akiandika riwaya hizi, uhuru wa kuikosoa serikali iliyokuwa

mamlakani haukuwepo na kwa hivyo, alilazimika kutumia ufumbaji kuwasilisha ujumbe

wake ili kuhepa rungu ya serikali. Pili, alikosomea na waandishi wengine, walimwathiri

katika matumizi ya mbinu ya ufumbaji katika uandishi wake. Tatu, kutokana na kazi hii, ni

dhahiri kuwa Mkangi alitumia mbinu ya ufumbaji kumzindua msomaji kuhusu athari za

utabaka, ubepari, unafiki wa viongozi, sheria na nafasi yake katika jamii, umuhimu wa utu na

usawa, umuhimu wa mapinduzi katika ujenzi wa jamii mpya, elimu na utafiti, mchango wa

vijana katika ujenzi wa taifa miongoni mwa mengine. Aidha, imebainika kuwa Mkangi

alitumia taswira, jazanda na istiari katika kufumba ujumbe wake. Hali kadhalika,

imedhihirika kuwa ufumbaji ulimsaidia Mkangi katika usawiri wa wahusika wake kwa

kuwapa majina ya majazi na lugha ya kimafumbo. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia

Amali ambayo hupima umuhimu wa kitu kwa kuangalia matokeo ya matumizi ya hicho kitu.

Nadharia hii hujishughulisha zaidi na matokeo na athari za hayo matokeo. Kwa hivyo,

tumechunguza umuhimu wa ufumbaji kwa kuangalia matokeo na athari zake kwenye kazi za

Mkangi. Utafiti huu ulifanyiwa maktabani na kwenye mtandao. Kwa jumla mafumbo

yamechunguzwa na kuwekwa katika makundi kutegemea namna yalivyojengwa. Ukusanyaji

wa data ulifanywa kupitia kwa mbinu ya uchanganuzi wa matini au yaliyomo. Data

iliyokusanywa na kuchanganuliwa imewasilishwa kwa njia ya maelezo. Utafiti huu ni

muhimu kwa njia mbalimbali. Kwanza, utakuwa kama mwongozo kwa waandishi wa

baadaye kuandika kazi nzuri zaidi kimafumbo. Pili, utawasaidia wasomi kuelewa kazi hizi

zilizoandikwa kimafumbo. Tatu, utafiti huu unachangia pia katika kuangalia riwaya za

Kiswahili kitaaluma hasa kwa misingi ya ufumbaji kwa kutumia Nadharia Amali.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

AYIERA, E (2021). Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/ufumbaji-katika-riwaya-za-katama-mkangi

MLA 8th

AYIERA, ELIJAH "Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi" Afribary. Afribary, 08 May. 2021, https://afribary.com/works/ufumbaji-katika-riwaya-za-katama-mkangi. Accessed 05 May. 2024.

MLA7

AYIERA, ELIJAH . "Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi". Afribary, Afribary, 08 May. 2021. Web. 05 May. 2024. < https://afribary.com/works/ufumbaji-katika-riwaya-za-katama-mkangi >.

Chicago

AYIERA, ELIJAH . "Ufumbaji Katika Riwaya Za Katama Mkangi" Afribary (2021). Accessed May 05, 2024. https://afribary.com/works/ufumbaji-katika-riwaya-za-katama-mkangi