Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya

Subscribe to access this work and thousands more

 

IKISIRI

Utafiti huu ulijikita katika kutathmini utayari wa Wakenya katika utekelezaji wa

sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi nchini Kenya. Utafiti ulilenga

wakaazi wa mji wa Nairobi hasa katika ofisi za shughuli za kiutawala na vyombo

vya habari vinavyopatikana humo. Utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya

Kiswahili umeathiriwa na mambo mbalimbali. Baadhi ya mambo hayo ni kama

vile: hadhi ambayo lugha hii imepewa, manufaa ya lugha hii miongoni mwa

athari nyingine. Malengo ya utafiti huu yalikuwa; kubaini iwapo kuna utayari

katika kutekeleza sera ya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi. Na namna utayari

huu utakavyosaidia katika kuimarisha sera hii mpya ya lugha ya Kiswahili hasa

katika urasmi wake, kuchunguza changamoto zinazokabiliwa katika shughuli za

kiutawala na vyombo vya habari kuhusu hadhi mpya ya lugha ya Kiswahili na

mwisho kutambua ni vipi utayari wa utekelezaji katika sera hii unavyoweza

kutekelezwa ili kuweza kufanikisha lengo lake la kuwa lugha rasmi. Utafiti huu

ulitumia mitazamo miwili ya upangaji wa lugha. Tulizingatia upangaji lugha

kihadhi ambao huzingatia juhudi zinazochukuliwa ili kubadilisha matumizi na

majukumu ya lugha katika jamii na mtazamo wa upangaji lugha kifahari

unaolenga kutoa mielekeo chanya ya kisaikolojia ambayo ni muhimu ikiwa

kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangaji lugha. Utafiti huu

uliongozwa na Nadharia ya Utekelezaji iliyoasisiwa na Spencer (1971). Utafiti

wa kina nyanjani ulifanywa ili kubaini ni changamoto zipi ambazo zinakumba

utayari wa utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi. Mtafiti

alitumia sampuli finyu ili kupata matokeo bora zaidi. Data ilikusanywa nyanjani

kwa kutumia hojaji na mahojiano ili kubaini mambo yanayohusu utayari wa

utekelezaji wa sera ya lugha ya Kiswahili hasa baada ya lugha hii kufanywa

lugha rasmi. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia programu ya SPSS.

Kutokana na matokeo ya utafiti ilidhihirika kuwa hakuna usawa katika matumizi

ya lugha yaKiswahili na ile ya Kiingereza. Utafiti ulionyesha kuwa lugha ya

Kiswahili ilitumika sana katika idara ya polisi, Kiingereza kilitumika sana katika

vyombo vya habari. Hata hivyo, ni bora wabunge wapitishe miswada

inayohusiana na lugha ya Kiswahili ili iwe sheria. Utafiti huu utasaidia wadau

wanaohusika na maswala ya sera ya lugha na kuweka mikakati ya kuhakikisha

kuwa inatekelezwa. Mapendekezo yaliyofanywa na mtafiti yakizingatiwa na

kutekelezwa, hadhi ya lugha ya Kiswahili itaweza kuwa bora katika sekta

zilizofanyiwa utafiti kwa nchi nzima kwa ujumla.

Subscribe to access this work and thousands more
Overall Rating

0

5 Star
(0)
4 Star
(0)
3 Star
(0)
2 Star
(0)
1 Star
(0)
APA

NAIROBI, K (2021). Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya

MLA 8th

NAIROBI, KAUNTI "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya" Afribary. Afribary, 01 Jun. 2021, https://afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya. Accessed 28 Mar. 2024.

MLA7

NAIROBI, KAUNTI . "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya". Afribary, Afribary, 01 Jun. 2021. Web. 28 Mar. 2024. < https://afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya >.

Chicago

NAIROBI, KAUNTI . "Utayari Wa Wakenya Katika Utekelezaji Wa Sera Ya Lugha Ya Kiswahili Kama Lugha Rasmi Nchini Kenya" Afribary (2021). Accessed March 28, 2024. https://afribary.com/works/utayari-wa-wakenya-katika-utekelezaji-wa-sera-ya-lugha-ya-kiswahili-kama-lugha-rasmi-nchini-kenya