SHUKURANI
Kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia uzima wa afya katika kipindi chote cha masomo yangu hadi kuikamilisha tasinifu hii katika muda uliopangwa. Pia ninawashukuru wale wote walioshirikiana na mimi mwanzo hadi mwisho wa tasinifu hii. Kwa uchache ninapenda kuwapa shukurani zangu za dhati kwa kuwataja hawa wafuatao; Kwanza, ninapenda kumshukuru msimamizi wangu, Dkt. Zuhura A. Badru, ambaye alijikubalisha kuniongoza licha ya majukumu mengi ya kiofisi na kifamilia yaliyomkabili lakini alijitolea na kunishauri vizuri hatua kwa hatua hadi kuikamilisha kazi hii. Mwenyezi Mungu amjaaliye afya njema na umri mrefu wenye kheri ili azidi kuwatumikia na wengine. Shukurani zangu zingine ziende kwa Dkt. Aginiwe Nelson Sanga ambaye alinivumilia na kunishauri na kuniongoza kila wakati hadi kuikamilisha tasinifu hii. Pia watafitiwa wangu wote niliofanya nao mahojiano na kushirikiana na mimi Mungu awalipe kila la kheri. Napenda vilevile kuwashukuru wahadhiri wote waliotufundisha na waliotusimamia katika mambo mbalimbali ya kitaaluma katika kiwango hiki cha shahada ya umahiri, pamoja na wanafunzi wenzagu. Kwa kumalizia ninapenda shukurani hizi zifike kwa familia yangu yote kwa kunivumilia kipindi chote cha masomo mbali na hali ngumu ya maisha waliokabiliana nayo.
MKOMBE, V (2021). Mdhihiriko Wa Mwendo Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Diwani Za Wasakatonge Na Kimbunga. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/mdhihiriko-wa-mwendo-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-katika-diwani-za-wasakatonge-na-kimbunga
MKOMBE, VUAI "Mdhihiriko Wa Mwendo Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Diwani Za Wasakatonge Na Kimbunga" Afribary. Afribary, 18 May. 2021, https://afribary.com/works/mdhihiriko-wa-mwendo-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-katika-diwani-za-wasakatonge-na-kimbunga. Accessed 22 Jan. 2025.
MKOMBE, VUAI . "Mdhihiriko Wa Mwendo Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Diwani Za Wasakatonge Na Kimbunga". Afribary, Afribary, 18 May. 2021. Web. 22 Jan. 2025. < https://afribary.com/works/mdhihiriko-wa-mwendo-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-katika-diwani-za-wasakatonge-na-kimbunga >.
MKOMBE, VUAI . "Mdhihiriko Wa Mwendo Katika Ushairi Wa Kiswahili: Mifano Kutoka Katika Diwani Za Wasakatonge Na Kimbunga" Afribary (2021). Accessed January 22, 2025. https://afribary.com/works/mdhihiriko-wa-mwendo-katika-ushairi-wa-kiswahili-mifano-kutoka-katika-diwani-za-wasakatonge-na-kimbunga