IKISIRI
Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa ni kuchunguza matumizi ya Kiswahili katika
ufunzaji na ujifunzaji wa shule za chekechea. Utafiti ulifanywa katika Manispaa
ya Webuye katika Wilaya ya Bungoma Mashariki, Mkoani Magharibi nchini
Kenya. Sampuli ya watafitiwa iliteuliwa kwa kutumia mbinu za mfumo sahili na
njia nasibu sahili. Idadi ya wasimamizi 19, walimu 19 na wazazi 19 wa shule za
chekechea walikuwa sehemu ya sampuli.
Data ilikusanywa kupitia hojaji, masaili na kiongozi cha uchunzaji. Data
ilichanganuliwa kiidadi na kimaelezo. Michoro, chati na grafu zilitumiwa
kuwasilisha data iliyokusanywa, utafiti uliongozwa na nadharia ya uamilifu ya
Halliday (1970). Nadharia inafafanua kuwa lugha ndiyo nguzo muhimu katika
ufunzaji na ujifunzaji.
Utafiti uligundua kuwa lugha ya Kiingereza na lugha ya Kienyeji zilitumika katika
muktadha mmoja na lugha ya Kiswahili. Pia ilifichuliwa kuwa hakukuwa na
nyenzo na vielelezo katika lugha ya Kiswahili. Vilevile hakukuwa na maandalizi
ya semina katika matumizi ya lugha ya Kiswahili. Utafiti ulifichua kuwa wazazi
wengi wa chekechea hawakuunga mkono matumizi ya lugha ya Kiswahili. Japo
kulikuwa na vikwazo, Kiswahili ndiyo lugha iliyokuwa maarufu katika shule za
chekechea. Mtafiti anapendekeza kuwa jumuiya nzima ya chekechea izingatie
sera rasmi ya lugha ambayo inasisitiza matumizi ya lugha sambazi.
Lugha ya Kiswahili inastahili kuimarishwa, kukuzwa kama lugha ya kufundishia
katika shule za chekechea za miji. Iwapo ni lazima lugha nyingine kutumika, ni
sharti iwe katika miktadha tofauti. Jumuiya nzima ya chekechea inapaswa
kuunda nyenzo na vielelezo vyenye maandishi katika lugha ya Kiswahili. K.I.E
ipange semina juu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili, kwa sababu walimu
watavumbua mikakati mipya itakayoendeleza lugha ya Kiswahili katika shule za
chekechea.
N., L (2021). Uchunguzi Wa Matumizi Ya Kiswahili Katika Ufunzaji Na Ujifunzaji Wa Shule Za Chekechea Katika Manispaa Ya Webuye, Kenya. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/uchunguzi-wa-matumizi-ya-kiswahili-katika-ufunzaji-na-ujifunzaji-wa-shule-za-chekechea-katika-manispaa-ya-webuye-kenya
N., LIAMBILA "Uchunguzi Wa Matumizi Ya Kiswahili Katika Ufunzaji Na Ujifunzaji Wa Shule Za Chekechea Katika Manispaa Ya Webuye, Kenya" Afribary. Afribary, 08 May. 2021, https://afribary.com/works/uchunguzi-wa-matumizi-ya-kiswahili-katika-ufunzaji-na-ujifunzaji-wa-shule-za-chekechea-katika-manispaa-ya-webuye-kenya. Accessed 22 Jan. 2025.
N., LIAMBILA . "Uchunguzi Wa Matumizi Ya Kiswahili Katika Ufunzaji Na Ujifunzaji Wa Shule Za Chekechea Katika Manispaa Ya Webuye, Kenya". Afribary, Afribary, 08 May. 2021. Web. 22 Jan. 2025. < https://afribary.com/works/uchunguzi-wa-matumizi-ya-kiswahili-katika-ufunzaji-na-ujifunzaji-wa-shule-za-chekechea-katika-manispaa-ya-webuye-kenya >.
N., LIAMBILA . "Uchunguzi Wa Matumizi Ya Kiswahili Katika Ufunzaji Na Ujifunzaji Wa Shule Za Chekechea Katika Manispaa Ya Webuye, Kenya" Afribary (2021). Accessed January 22, 2025. https://afribary.com/works/uchunguzi-wa-matumizi-ya-kiswahili-katika-ufunzaji-na-ujifunzaji-wa-shule-za-chekechea-katika-manispaa-ya-webuye-kenya