IKISIRI
Utafiti huu ulihusu Korasi katika Tamthiliya ya Kiswahili: Mifano toka Tamthiliya
Teule za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, na Frowin Nyoni. Dhana ya korasi
imetumiwa ikimaanisha matendo, fikra au maneno ya kisanaa ayatoayo mtu au kikundi
cha watu katika kitendo cha kisanaa kwa njia ya uimbaji, uradidi, nathari na kuambatana
na vitendo. Matumizi ya mbinu hii ya korasi hayajatafitiwa wala kuhakikiwa vya
kutosha katika Fasihi ya Kiswahili. Hali hii inakifanya kipengele hiki kutojulikana sana
na wasomi na wanajamii wengi. Tamthiliya za waandishi teule zilizotafitiwa ni Kwenye
Ukingo wa Thim, Ngoma ya Ng’wanamalundi na Mabepari wa Bongo.
Utafiti huu ulifanyika maktabani kwa kiasi kikubwa. Vilevile mtafiti alifanikiwa
kuzungumza na wataalamu mbalimbali wa fasihi ili kupata mawazo komavu kuhusiana
na mada. Uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti uliongozwa na
Nadharia ya Mwitiko wa Msomaji kupitia nguzo yake kuu ya uhuru wa msomaji wa
kupata maana kutokana na uzoefu wake.
Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa kipengele cha korasi hutumika katika tamthiliya
kwa malengo mahususi na wala si kwa bahati nasibu tu. Mchango mpya ulioibuliwa na
utafiti huu ni: Kwanza, ni kupanua ufafanuzi wa dhana ya korasi. Pili, ni kuonyesha
nafasi ya korasi katika tamthiliya, hususani katika tamthiliya za waandishi teule. Tatu,
ubainishaji na uchambuzi wa dhima za korasi ambazo ni kutambulisha onyesho,
kuunganisha onyesho moja na jingine, kuwasilisha dhamira, kudhihirisha ujumi, kujenga
taharuki, kuleta ucheshi na kufunga onyesho. Hivyo, korasi hutumika kama nguzo katika
ujenzi na uendelezaji wa tamthiliya.
Kiloba, L (2021). Korasi Katika Tamthiliya Ya Kiswahili: Mifano Toka Tamthiliya Teule Za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, Na Frowin Nyoni. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/korasi-katika-tamthiliya-ya-kiswahili-mifano-toka-tamthiliya-teule-za-ebrahim-hussein-emmanuel-mbogo-na-frowin-nyoni
Kiloba, Leah "Korasi Katika Tamthiliya Ya Kiswahili: Mifano Toka Tamthiliya Teule Za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, Na Frowin Nyoni" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/korasi-katika-tamthiliya-ya-kiswahili-mifano-toka-tamthiliya-teule-za-ebrahim-hussein-emmanuel-mbogo-na-frowin-nyoni. Accessed 30 Nov. 2024.
Kiloba, Leah . "Korasi Katika Tamthiliya Ya Kiswahili: Mifano Toka Tamthiliya Teule Za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, Na Frowin Nyoni". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/korasi-katika-tamthiliya-ya-kiswahili-mifano-toka-tamthiliya-teule-za-ebrahim-hussein-emmanuel-mbogo-na-frowin-nyoni >.
Kiloba, Leah . "Korasi Katika Tamthiliya Ya Kiswahili: Mifano Toka Tamthiliya Teule Za Ebrahim Hussein, Emmanuel Mbogo, Na Frowin Nyoni" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/korasi-katika-tamthiliya-ya-kiswahili-mifano-toka-tamthiliya-teule-za-ebrahim-hussein-emmanuel-mbogo-na-frowin-nyoni