IKISIRI
Huu ni
utafiti uliofanywa juu ya ufasihi katika kasida za madrasa kutoka wilaya ya
Mjini Zanzibar kwa mwaka 2013. Tafiti mbalimbali zimefanyika kabla ya utafiti huu,
lakini zote hizo zimeelezea maana ya kasida, historia na dhima ya jumla ya kasida
ambayo ni kumsi fu mtume Muhammad (s.a.w) mfano Simiyu (2011:89) na Mulokozi
2011:14) 14). Dhana hiyo pia ime elezwa kabla na BAKI ZA (2010:147), Paden (2009),
Tuzin (2009) Al Mubarakpuri (2004:310), Ntarangwi (2004:67) na Mulokozi
(1996:70 Kwa kuchunguza kwa undani tafiti hizi zote hazijaelezea ufasihi
unaojitokeza katika kasida za madrasa.
Madhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza ufasihi unaojitokeza kati
ka kasida za
madrasa. Kama wasem avyo BAKIZA (2010:82) kuwa fasihi ni sanaa ya lugha.
Hivyo usanii wa kasida ni mbinu mbali mbali zilizotumika katika kasida za madrasa
zenye kudhihirisha ufundi au usanii wa lugha . Kwa mfano matumizi ya lugha, ujenzi
wa muundo, uteuzi wa mtindo na uibuaji wa dhamira.
Utafiti huu ni muhimu katika taaluma ya f
asihi simulizi hasa katika vipengele vya
fani na maudhui pamoja na kubainisha utendaji wa kasida za madrasa za wilaya ya
Mjini Zanzibar. Utafiti huu utawafaa wanazuoni wengine wanaotaka kufanya utafiti
zaidi kuhusu kasida. Matokeo ya utafiti huu ya takuwa k ianzio kwa yale masuala
ambayo hajashughulikiwa katika utafiti huu.
Mbinu shirikishi (kuangalia), mahojiano ya ana kwa ana na dodoso la maswali
zilitumika katika kukusanya data za utafiti huu. Hatimaye nadharia ya Ujumi wa
Kinudhuma ilitumika wakati wa kuw asilisha na kufafanua data za utafiti huu.
Mganga, N (2021). Ufasihi Katika Kasida Za Madrasa. Afribary. Retrieved from https://afribary.com/works/ufasihi-katika-kasida-za-madrasa
Mganga, Nawaje "Ufasihi Katika Kasida Za Madrasa" Afribary. Afribary, 26 Apr. 2021, https://afribary.com/works/ufasihi-katika-kasida-za-madrasa. Accessed 30 Nov. 2024.
Mganga, Nawaje . "Ufasihi Katika Kasida Za Madrasa". Afribary, Afribary, 26 Apr. 2021. Web. 30 Nov. 2024. < https://afribary.com/works/ufasihi-katika-kasida-za-madrasa >.
Mganga, Nawaje . "Ufasihi Katika Kasida Za Madrasa" Afribary (2021). Accessed November 30, 2024. https://afribary.com/works/ufasihi-katika-kasida-za-madrasa